Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dk. Shukuru Kawambwa, akizungumza kwenye mkutano wa kampeni, kumnadi mgombea nafasi ya mwenyekiti kupitia CCM kitongoji cha Magomeni B, Rajabu Swedy. (picha na Mwamvua Mwinyi) |
Meneja kampeni uchaguzi
mdogo kitongoji cha Magomeni B (CCM)alhaj Abdul Zahoro ,akimkaribisha
mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Dk. Shukuru Kawambwa kumnadi mgombea
kupitia CCM Rajabu Swedy. (picha na Mwamvua Mwinyi)
……………………………………………………………………..
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
MBUNGE wa jimbo la
Bagamoyo, mkoani Pwani, Dk. Shukuru Kawambwa, amesema anaendelea
kuivalia njuga changamoto ya maji inayokabili baadhi ya maeneo jimboni
hapo ikiwemo kitongoji cha Magomeni B.
Aidha ameeleza jitihada
alizozifanya kuhakikisha vijiji na vitongoji vinavyokabiliwa na
changamoto ya ukosefu wa nishati ya umeme ,vinaingizwa katika awamu ya
III ya umeme vijijini (REA) .
Dk. Kawambwa aliyasema
hayo, wakati akimnadi mgombea wa nafasi ya mwenyekiti kitongoji cha
Magomeni B ,Rajabu Swedy katika kampeni zinazoendelea kufanyika.
Alisema yeye ataweza kusimamia na kutatua changamoto mbalimbali kwa kushirikiana na viongozi kutoka CCM badala ya wapinzani.
“Ni mengi nayafanya na
mengine nikiendelea kuyafuatilia katika idara husika hivyo msifanye
makosa kuwapa ridhaa vyama vya upinzani bali mchagueni Swedy kuwa
mwenyekiti wenu”alisema dk. Kawambwa.
Dk. Kawambwa alisema endapo atachaguliwa mtu kutoka vyama vya upinzani atashindwa kufanya nae kazi kirahisi.
Hata hivyo alieleza
kwamba, kwasasa mabomba makuu ya usafirishaji maji yameshalazwa na
mtandao wa mabomba ukiendelea kutandazwa .
Alisema zoezi hilo litakapokamilika itasaidia kuondoa adha ya maji jimboni humo.
Dk.Kawambwa alisema
,anashirikiana na viongozi mbalimbali wa vitongoji, vijiji, madiwani
kufuatilia tatizo hilo,kwa kuzungumza na wizara husika na dawasco kujua
hatua zinazoendelea .
Kuhusu nishati ya umeme
alisema changamoto hiyo itakuwa historia baada ya vitongoji vyote
kuingizwa katika awamu ya tatu ya REA .
Nae katibu wa chama cha
mapinduzi (CCM),Kombo Kamote, alisema wananchi wa kitongoji cha
Magomeni B wamuamini Swedy kwani ana sifa na uwezo wa kuwaongoza.
Kamote aliwaasa wasijaribu kuchagua vyama visivyo na sera makini.
Diwani wa kata ya
Magomeni, Mwanaharusi Jarhuf, alisema halmashauri ya wilaya hiyo,
imepanga kujenga kisima kikubwa kitakachokuwa na uwezo wa kulisha maeneo
mengi ya wilaya ikiwemo Magomeni B.
Mwanaharusi alisema serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuwatua ndoo kichwani akinamama .
Meneja wa kampeni za
uchaguzi mdogo katika kitongoji hicho, alhaj Abdul Zahoro, aliwasihi
wananchi kujitokeza februari 19 kwenda kupiga kura.
Alhaj Zahoro alisema wasihadaike, wasidanganywe bali kiongozi makini ni Swedy kutoka CCM.
|
No comments:
Post a Comment