Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Mara imewapandisha
kizimbani Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo mjini Musoma, Swalala Mathayo
(40) na karani wa Mahakama hiyo, Charles Masatu (56) kwa tuhuma za kudai
na kupokea rushwa.
Mbele
ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Musoma, Richard Maganga, Mwendesha
Mashtaka wa Takukuru, Marshal Mseja, alidai watuhumiwa hao kwa pamoja
wanadaiwa kuomba na kupokea rushwa ya Sh 200,000.
Alidai
Hakimu Mathayo anatuhumiwa kwa makosa mawili ya kuomba na kupokea
rushwa,wakati karani Masatu anatuhumiwa kushiriki katika kuiomba rushwa
hiyo.
Mseja
alidai chanzo cha madai hayo ya rushwa ni kuwa hakimu huyo alitoa
hukumu ya kifungo cha miaka miwili kwa Magdalena Aloyce (29) mkazi wa
mtaa wa Makongora mjini Musoma.
Alidai
kwa vile mtuhumiwa alifungwa akiwa na mtoto mdogo wa miezi 10 na
kuwaacha wengine wawli bila uangalizi, ndugu zake walimfuata mkuu wa
gereza na kuomba mfungwa huyo apewa kifungo cha nje aweze kuhudumia
familia yake ambayo inamtegemea.
Ndugu
walipewa maelekezo na mkuu wa magereza kwenda kwa ofisa wa ustawi wa
jamii na walipofika walihudumiwa na kujaziwa fomu namba 12 kwa mujibu wa
Sheria ya Kutumikia Jamii, alisema.
Alisema fomu hiyo ilitakiwa kuidhinishwa na hakimu aliyetoa hukumu hiyo.
Mseja
alidai hakimu huyo hakuweza kufanya hivyo bali alitengeneza mianya ya
kudai rushwa kwa kumuhusisha karani wake na hapo ndipo ndugu hao
walipotoa taarifa Takukuru na kuwekwa mtego na hatimaye kukamatwa na
rushwa hiyo ya Sh 200,000.
Watuhumiwa hao walikana mashitaka na wapo nje kwa dhamana hadi Machi 21 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
|
February 15, 2017
HAKIMU,KARANI KORTINI KWA KWA TUHUMA ZA RUSHWA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment