Na. Benedict Liwenga-WHUSM.
SERIKALI imesema kwamba tatizo la
maradhi yasiyoambukiza yakiwemo magonjwa ya akili yamekuwa yakiongezeka
siku hadi siku huku vyanzo vyake vikiwa ni pamoja na urithi, matumizi ya
madawa ya kulevya, pombe, matatizo ya kisaikolojia pamoja na hali ngumu
ya maisha.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini
Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipokuwa akizindua Bodi ya Hospitali ya Mrembe
Mkoani hapo.
Akiongea na mbele ya Watendaji wa
Bodi hiyo, wageni waalikwa pamoja na Viongozi wa hospitalini hapo,
Waziri Ummy amesema kuwa, kundi lililoathirika Zaidi na kdhai hiyo ni
vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa, ambapo alitaja taarifa ya Shirikala
Afya Ulimwenguni (WHO) ya mwaka 2016n inayoonyesha takribani watu
milioni 15.3 Duniani wanapata matatizo ya kiafya yatokanayo na matumizi
ya dawa za kulevya pamoja na matumizi ya pombe kupita kiasi.
“Matatizo haya yamekuwa
yakisababisha vifo milioni 3.3 kila mwaka Duniani kote, hata hivyo
taarifa ya Wizata yangu inaonyesha kwamba idadi ya watu wanaougua
magonjwa ya akili inaongezeka kwa kasi kubwa kutoka wagonjwa 136,710
mwaka 2011/2012 hado wagonjwa 448,997 mwaka 2015/2016”, alisema Ummy.
Ameongeza kuwa, takwimu za
hospitali ya Mirembe zinaonyesha kuwa, katika kipindi cha miaka mine
kuanzia mwaka 2012 hadi 2016, jumla ya wagonjwa Zaidi ya 60,000 wenye
magonjwa ya akili na waathirika wa dawa za kulevya walipatiwa huduma za
afya na utengamao.
Aidha, kwa kutambua majukumu
makubwa ya hospitali hiyo na kutatua changamoto zinazohusiana na
magonjwa hayo, Serikali imeamua kuunda Bodi ya hospitalini hapo lengo
likiwa ni kutekeleza dhana ya Utawala Bora na Utoaji wa Huduma Bora za
Afya ya Akili kwa mujibu wa mapango mkakati na sera za nchi.
“Ninayo furaja leo kushiriki nanyi
katika uzinduzi wa Bodi hii ya Hospitali ya Afya ya Akili Mirembe, na
bodi hii itaongozwa na Mwenyekiti pamoja na Wajumbe waliouteuliwa kutoka
maeneo mbaimbali ya kiujuzi hapa nchini”, alisema Waziri Ummy.
Amesema kuwa, bodi hiyo itakuwa na
majukumu mbalimbali yakiwemo kusimamia utendaji wa hospitali hiyo na
Taasisi ya Isanga, kuhakikisha kuwa Sheria ya uanzishwaji wa hospitali
inapatikana kwa wakati, kushauri kuhusu muundo wa hospitali, kuunda
kamati ndogo ndogo, kushauri kuhusu mpango wa muda mrefu ili kuboresha
huduma pamoja na kushauri jinsi ya kupunguza gharama za uendeshaji
hospitalini hapo.
Sambamba na kuzindua bodi hiyo,
Waziri Ummy ameitaka jamii kushirikiana na Serikali katika kupiga vita
matumizi ya madawa ya kulevya hususan kwa vijana ili nguvu kazi ya Taifa
isizidi kupotea.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi
hiyo, Profesa Gadi Kilonzo amempongeza Waziri Ummy na kwa kuzindua bodi
hiyo na amemuhakikishia kuwa bodi hiyo itatekeleza maagizo yote pamoja
na majukumu iliyopewa ili kuboresha utendaji kazi hospitakini hapo.
“Dhama uliyotupa sisi Wajumbe wa
Bodi ni kubwa, tunaieheshimu sana na pia nakuahidi kuwa, tutatekeleza
kwa bidii majukumu yote ya kuisimamia hospitali hii, tutajitahidi kwa
uwezo wetu wote kutatua changamoto za hospitali hii kwa kushirikiana na
wadau wengine wa afya kupitia Wizara yako, pia tunashukuru kwa vifaa vya
kazi ulivyotupatia kwa ajili ya kutumia wakati wa utendaji wetu”,
alisem Kilonzo.
Wajumbe waliochaguliwa kuunda bodi
hiyo ni Profesa Gadi Kilonzo ambaye ndio Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dkt.
Erasmus Mndeme ambaye ni Katibu wa Bodi na Mganga Mkuu wa Hospitali ya
Mirembe, Dkt. Mpona Boniventura ambaye ni Mwakilishi kutoka chuo Kikuu
cha Dodoma, Profesa Joseph Mbatia, Ndugu John Sipendi, Ndugu Ernest
Kabohola, Ndugu Jane Magembe pamoja na Ndugu Clavery Lyela.
|
February 8, 2017
WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA BODI YA HOSPITALI YA MIREMBE KUKABILIANA NA TATIZO LA MAGONJWA YA AKILI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment