Mfanyabiashara
maarufu na Mwenyekiti wa Club ya soka ya Yanga Yusuph Manji amekua
akishikiliwa na Polisi kituo cha kati Dar es salaam toka Alhamisi ya
February 9 2017 baada ya kwenda kuhojiwa kutokana na kutajwa na Mkuu wa
Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwenye orodha ya watu 65 kwenye
sakata la dawa za kulevya.
Jana
jioni Mfanyabiashara huyo alichukuliwa na gari la kubebea Wagonjwa
lenye namba za usajili za DFP na alionekana akitembea na kuingia kwenye
gari hilo (Land Cruise Nyeupe) yeye mwenyewe bila kubebwa au kusaidiwa
huku gari lake aina ya Range Rover likitangulia mbele na watu wengine.
Baada
ya gari hilo kumchukua msafara huo ulikwenda moja kwa moja kwenye
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Muhimbili Dar es salaam ambako watu
mbalimbali wanaosumbuliwa na moyo hupata matibabu.
|
February 13, 2017
YUSUF MANJI ALIVOCHUKULIWA NA GARI LA WAGONJWA POLISI NA KISHA KUPELEKWA HOSPITALI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment