Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
NBC Tanzania Bw. Edward Marks, akizungumza jambo wakati wa maadhimisho
ya Benki yake kutimiza miaka 50, tukio lililofanyika Mjini Dodoma Jana
usiku.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
ya Benki ya NBC, Bw. Nehemiah Mchechu, akitaja mafanikio makubwa
yaliyofikiwa na Benki hiyo, wakati wa uzinduzi rasmi wa maadhimisho ya
Benki hiyo kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake, tukio lililofanyika
katika ukumbi wa Hoteli ya Morena, Mjini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Josephat Kandege, akipokea tuzo kwaniaba
ya wabunge, tuzo iliyotolewa na NBC kutambua mchango wa Bunge katika
kuanzishwa kwa Benki hiyo miaka 50 iliyopita.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Mpango (Mb), akionyesha alama ya dole! akifurahia gawiwo la
shilingi bilioni 1.7 zilizotolewa na NBC kwa Serikali, ambayo inamiliki
asilimia 30 za hisa katika Benki hiyo
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Mpango (Mb), akishukuru baada ya kupokea gawiwo la shilingi
bilioni 1.7 zilizotolewa na NBC kwa Serikali, ambayo inamiliki asilimia
30 za hisa katika Benki hiyo
Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee Samwel
Malecela, akitoa neon la shukurani kwenye hafla ya Benki ya Taifa ya
Biashara (NBC) kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake, sherehe
zilizofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Morena mjini Dodoma.
(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
Benny Mwaipaja, WFM-Dodoma
Benki ya Taifa ya Biashara
(NBC) kwa mara ya kwanza imetoa gawiwo la shilingi bilioni 1.7 kwa
Serikali ambayo inamiliki asilimia 30 ya hisa za Benki hiyo.
Hundi kifani ya kiasi hicho
cha fedha alikabidhiwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip
Mpango (Mb), kwaniaba ya Waziri Mkuu, katika tukio la Benki hiyo
kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake, tukio lililofanyika katika
Hoteli ya Morena Mjini Dodoma.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa
Benki hiyo kutoa gawiwo kwa wanahisa wake katika kipindi cha miaka 9
baada ya kuanza kupata faida ya uwekezaji wake hapa nchini.
Dkt. Mpango aliishukuru Benki
hiyo kwa kuanza kutoa gawiwo kwa wanahisa wake baada ya ukame wa muda
mrefu na kuelezea matumaini yake kwamba kiasi cha gawiwo kitaongezeka
zaidi miaka ijayo.
Hata hivyo alizitaka Benki
zote hapa nchini kupunguza riba za mikopo inazotoza kwa wateja wao hasa
baada ya Benki Kuu ya Tanzania-BOT kupunguza riba za mikopo kwa mabenki
kutoka asilimia 16 hadi asilimia 12.
Alizitaka pia taasisi za fedha
nchini, kuwekeza fedha katika kutekeleza Mpango wa Pili wa Taifa wa
Maendeleo kwa njia ya mikopo kwa wateja wao kwa ajili ya ujenzi wa
viwanda vitakavyosisimua uchumi na kukuza ajira nchini.
Alipongeza pia juhudi
zilizofanywa na Benki hiyo kufanya uwekezaji mkubwa kwenye mtandao wa
malipo ya kielektroniki ikiwa ni maagizo ya Serikali kwamba malipo yote
ya Serikaloi yafanyike benki au kupitia miamala ya kielektroniki
“Nimefurahi kuthibitishiwa
kwamba, kutoka tarehe 1 Julai 2016 hadi kufikia tarehe 30 Aprili 2017,
NBC imekusanya fedha za Serikali na kuzituma kielektroniki katika
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) jumla ya Shillingi Billioni 991”
aliongeza Dkt. Mpango.
Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa Benki hiyo, Nehemiah Mchechu, alieleza Mkakati wa Benki
hiyo ya tatu kwa ukubwa hapa nchini ikitanguliwa na Benki za NMB na
CRDB, huku ikiwa imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi trilioni 1,
kwamba imejipanga kusogeza huduma zake kwa wananchi na wafanyabiashara
wa kati na wa chini kabisa.
“Mwaka jana Benki yetu imepata
faida ya zaidi ya shilingi bilioni 13 na katika mkutano Mkuu wa
wanahisa tuemekubaliana kutoa gawiwo kwa wawekezaji” aliongeza Bw.
Mchechu.
No comments:
Post a Comment