Simba wanatakiwa
kushinda zaidi ya mabao nane katika mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu huku
wakiomba Yanga ipoteza kwa zaidi ya mabao matano dhidi ya Mbao FC mjini
Mwanza ili wao wawe mabingwa.
Lakini hiyo
haiwakatishi Simba tamaa na hawataki kusikia Yanga wakitangazwa kuwa
mabingwa kabla ya mechi yao ya mwisho wao wakiwavaa Mwadui FC jijini Dar
es Salaam.
Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesisitiza bado wanataka kuona matokeo hadi mechi ya mwisho.
“Sisi tunajua bingwa bado hajapatikana na tutaona hadi katika mechi ya mwisho. Tutapambana hadi tone la mwisho.
“Hatuwezi kukata tamaa, huu ni mpira na vijana wako vizuri kabisa,” alisema akionyesha kujiamini.
Endapo mechi ya
mwisho Yanga atakubali kufungwa atakuwa na pointi 68 sawa na Simba ambao
viongozi bado wanaamini kuwa pointi tatu walizopokonywa dhidi ya Kagera
Sugar zitarudishwa kwani wanataka kwenda FIFA kudai pointi zao na
watakuwa na pointi 71.
No comments:
Post a Comment