Rais wa Chuo cha Ustawi wa Jamii,
Yohana Mabena akizungumza wakati wa kuwatambulisha warembo wao kwa
wadhamini wakuu, kampuni ya Mabibo Beer. Kulia ni msemaji wa kampuni ya
Mabibo Beer, Andrea Missama na kushoto kwa Mabena ni Waziri wa Michezo
wa Ustawi, Ashura Jingu. Nyuma ni warembo wa miss Ustawi 2017.
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi
kipya nchini, Ben Paul akizungumza akizungumza wakati wa kutambulishwa
kuwa msanii wa kutumbuiza katika mashindano Miss Ustawi 2017
yaliyopangwa kufanyika Ijumaa (Mei 19) kwenye ukumbi wa King Solomon
uliopo Namanga, jijini.
Miss Ustawi anayemaliza muda wake
Evelyn Andrew akizungumza wakati wa utambulisho wa warembo hao kwa
wadhamini wakuu. Evelyn anavua taji hilo, Ijumaa (Mei 19) wakati wa
mashindano ya kumsaka mrembo wa chuo hicho kwenye ukumbi wa King Solomon
uliopo Namanga.
Warembo wakiwa katika picha ya
pamoja na Miss Ustawi anayemaliza muda wake, Evelyn Andrew. Warembo hao
watapambana Ijumaa (Mei 19) wakati wa mashindano ya kumsaka mrembo wa
chuo hicho kwenye ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga.
…………………………..
Na Mwandishi wetu
Mwanamuziki nyota wa kizazi kipya
nchini, Ben Paul atatumbuiza katika mashindano ya kumsaka mrembo wa Chuo
cha Ustawi wa Jamii (Miss Ustawi) yaliyopangwa kufanyika Ijumaa (Mei
19) kwenye ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga jijini.
Mratibu wa mashindano hayo,
Catherine Boniface alisema kuwa Paul ambaye anatamba na wimbo wa Moyo
Machine, Phone na nyinginezo nyingi, pia atatambulisha wimbo wake mpya
aliomshirikisha mwanamuziki nyota nchini, Darasa.
Mashindano hayo yamedhaminiwa na
kinywaji cha Windhoek, yatashirikisha jumla ya warembo 12 ambao walikaa
kambini kwa muda wa wiki mbili wakijifua chini ya mwalimu wao, Clara
Michael na matron, Catherine Boniface.
Warembo ambao wamepitishwa na
kamati ya mashindano hayo ni Fatma Kivea, Elice Mwakajila, Melody
Thomas, Diana Mwaibula, Hapifania Shedoekulu, Careen Kileo. Wengine ni
Angelina Michael, Ruth Deogratius, Consolator Samwel, Loyce Jeck na
Elizabeth Julius.
Washindi watatu wa mashindano
hayo watapata nafasi ya kushindana katika shindano la warembo wa elimu
ya juu (Miss Higher Learning Institution) ambapo warembo watatu wa
kwanza watafuzu katika mashindano ya Miss Tanzania mwaka huu.
Mratibu wa mashindano hayo,
Catherine Boniface alisema kuwa warembo watapanda jukwaani wakiwa
wanashindania vazi la ubunifu, ufukweni na usiku na warembo watano
watakaopita katika mchujo wa kwanza watajibu maswali.
“Morali ya warembo ipo juu, kila
mmoja ni mshindi, lengo letu ni kushinda taji la vyuo vya elimu ya juu
na kutwaa taji la Miss Tanzania kwa mara ya kwanza katika historia ya
mashindano ya urembo nchini,” alisema Catherine.
Msemaji wa kampuni ya Mabibo Beer
inayodhamini shindano hilo, Andrea Missama amesema kuwa wameamua
kudhamini shindano hilo kama sehemu ya kampuni yao kukuza vipaji na
kazi za jamii.
Missama amesema kuwa warembo wengi
wamejitokeza kushindania taji hilo ambalo mshindi wake atakiwakilisha
chuo hicho katika mashindano ya urembo ya vyuo vya elimu ya juu
No comments:
Post a Comment