Mchoraji Nembo ya Taifa , Mzee
Francis Maige Kanyasu akiwa katika Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali
Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake. Mzee
Kanyasu amefikishwa leo MNH akitokea Hospitali ya Amana.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya
Dharura na Ajali ambaye pia ni Mkuu wa Idara hiyo Juma Mfinanga
akimuhudumia Mzee Kanyasu mara baada ya kufikishwa Hospitali ya Taifa
Muhimbili.
Dar es salaam 25-05-2017
Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH- imeanza kumfanyia uchunguzi mchoraji wa Nembo ya Taifa , Mzee Francis Maige Kanyasu .
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya
Dharura na Ajali Dk. Juma Mfinanga amesema Mzee Kanyasu amechukuliwa
leo asubuhi kutoka Hospitali ya Amana ambako alipelekwa jana na majirani
zake na kupatiwa matibabu ya awali.
‘’ Tumemchukua kutoka Hospitali ya
Amana baada ya kupata habari zake kwenye vyombo vya habari kuwa hali
yake kiafya sio nzuri hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa MNH , Profesa
Lawrence Museru akatuagiza tumfuate ili apatiwe matibabu hapa Muhimbili
‘’ Amesema Dk. Juma.
‘’ Wenzetu wa Hospitali ya Amana
wamemfanyia uchunguzi wa awali na wakatueleza shida yake kubwa ni kukosa
nguvu na kushindwa kutembea hivyo tumemleta hapa Idara ya magonjwa ya
Dharura na Ajali kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Baada ya uchunguzi
tutamuanzishia tiba haraka kwa kushirikiana na Idara zingine hapahapa
MNH.’’ Amesema Dk. Juma.
Kwa mujibu wa Dk. Juma kukosa lishe , mazingira magumu pamoja na umri kunasababisha mtu kupata magonjwa mbalimbali.
No comments:
Post a Comment