Timu ya Taifa ya
vijana chini ya umri wa Miaka 17, Serengeti Boys, leo Jumatatu
inafungua pazia lake katika mashindano ya Kombe la Afrika kwa Vijana,
kwa kumenyana na Mali katika michuano hiyo inayofanyika nchini Gabon.
Serengeti Boys ipo Kundi B, pamoja na timu nyingine za Angola na Niger ambazo nazo zitakuwa kibaruani leo.
Akizungumza kwa njia
ya simu jana, kocha mkuu wa kikosi hicho, Bakari Shime, alisema kuwa
kikosi chake kipo vizuri na kimejiandaa vya kutosha kuwakabili vijana wa
Mali kwenye mchezo huo wa kwanza.
“Kikosi kipo vizuri
na tumejipanga kuikabili vilivyo timu ya Mali kwani tunataka
kuwafurahisha Watanzania kwa kutowaangusha na naomba wazidi kutuombea,”
alisema Bakari Shime.
Huku timu hiyo ikipata pigo baada ya Nahodha Abas Makamba amevunjika mguu kwa hiyo ataweza kukosa michuano yote
No comments:
Post a Comment