Kamishna
wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (wa pili kutoka
kulia), akijibu maswali mbalimbali kutoka kwa wachimbaji wadogo wa
madini wa eneo la Mererani, wakati wa mafunzo maalum kuhusu usalama
migodini yaliyofanyika hivi karibuni. Wengine pichani (kutoka kulia) ni
Mkaguzi Mkuu wa Migodi Tanzania, Mhandisi Ally Samaje, Kamishna Msaidizi
wa Madini Kanda ya Kaskazini, Adam Juma na Fundi Sanifu Migodi kutoka
Ofisi ya Madini Dar es Salaam, Stanslaus Basheka.
Mkaguzi
Mkuu wa Migodi Tanzania, Mhandisi Ally Samaje, akiwasilisha mada kuhusu
Usalama, Afya na Utunzaji wa Mazingira katika Migodi ya Wachimbaji
Wadogo wa Madini, wakati wa mafunzo maalum kwa wachimbaji wadogo wa eneo
la Mererani yaliyozinduliwa rasmi hivi karibuni.
Fundi
Sanifu Migodi kutoka Ofisi ya Madini Dar es Salaam, Stanslaus Basheka,
akiwasilisha mada kuhusu Matumizi salama na utunzaji wa baruti migodini,
wakati wa mafunzo maalum kwa wachimbaji wadogo wa madini wa eneo la
Mererani hivi karibuni.
Ofisa
wa Sheria kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Hadija Ramadhan,
akiwasilisha mada kuhusu Ufafanuzi wa Sera ya Madini ya Mwaka 2009,
Ufafanuzi wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na Kanuni zake za Mwaka
2010, wakati wa mafunzo maalum kwa wachimbaji wadogo wa madini wa eneo
la Mererani hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment