Klabu ya Yanga imepigwa faini ya
sh. 1,000,000 (milioni moja) kutokana na timu yake kutoingia vyumbani
wakati wa mechi hiyo iliyochezwa Mei 9, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Adhabu hiyo imetolewa kwa
mujibu wa Kanuni ya 14(48) ya Ligi Kuu. Uamuzi huo umezingatia pia kuwa
Yanga imekuwa ikirudia kosa hilo mara kwa mara.
Mechi namba 225 (JKT Ruvu 0 Vs Majimaji 1).
Timu ya Majimaji haikuingia
vyumbani wakati wa mapumziko katika mechi hiyo iliyofanyika Mei 13, 2017
katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Kutokana na timu hiyo kurudia
kufanya kosa hilo, klabu ya Majimaji imepigwa faini ya sh. 1,000,000
(milioni moja). Adhabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya 14(48) ya Ligi
Kuu.
Mechi namba 230 (Kagera Sugar 2 Vs Mbao FC 0).
Klabu ya Mbao imepigwa faini ya
sh. 500,000 (laki tano) kutokana na timu yake kutoingia vyumbani wakati
wa mechi hiyo iliyochezwa Mei 13, 2017 katika Uwanja wa Kaitaba mjini
Bukoba. Adhabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya 14(48) ya Ligi Kuu.
Mechi namba 231 (Yanga 2 Vs Mbeya City 1).
Timu zote mbili hazikupita kwenye
mlango rasmi wakati wa kuingia uwanjani katika mechi hiyo iliyochezwa
Mei 13, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Hivyo, kila klabu
imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na kitendo hicho,
uamuzi ambao umezingatia Kanuni ya 14(48).
Pia klabu ya Yanga imepigwa
faini ya sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kutoingia vyumbani kwenye
mechi hiyo. Adhabu hiyo pia imezingatia Kanuni ya 14(48) ya Ligi Kuu.
Mechi namba 236 (Mbao FC 1 Vs Yanga 0).
Klabu ya Yanga imepigwa faini ya
sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kupita mlango usio rasmi katika mechi
hiyo iliyofanyika Mei 20, 2017 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(48) ya Ligi
Kuu.
Pia Yanga imepigwa faini ya
sh. 1,500,000 (milioni moja na laki tano) kwa kutoingia vyumbani. Adhabu
hiyo imezingatia Kanuni ya 14(8) ya Ligi Kuu. Vilevile klabu hiyo
imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na kuonyesha vitendo
vinavyoashiria ushirikiana. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni
ya 42(1) ya Ligi Kuu.
Washabiki wa Yanga walivunja
uzio wa ndani (fence) wa upande wa Magharibi wakati wakiingia uwanjani
kusherehekea ubingwa wa timu hiyo. Hivyo, klabu ya Yanga imeagizwa
kulipa gharama za uharibifu huo uliofanywa na washabiki wake, uamuzi
ambao umezingatia Kanuni ya 42(3) ya Ligi Kuu.
Nayo klabu ya Mbao FC imepigwa
faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na washabiki wake kuingia
uwanjani kushangilia baada ya timu yao kupata ushindi.
Wachezaji Deus Kaseke, Simon
Msuva na Obrey Chirwa wa Yanga wamesimamishwa kucheza mechi za Ligi Kuu
wakati wakisubiri suala lao la kumsukuma na kumwangusha Mwamuzi Ludovic
Charles kusikilizwa na kutolewa uamuzi na Kamati ya Nidhamu ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Walifanya kitendo hicho katika
mechi hiyo dhidi ya Mbao FC iliyofanyika Mei 20, 2017 kwenye Uwanja wa
CCM Kirumba jijni Mwanza. Uamuzi wa Kamati umezingatia Kanuni ya 9(5) ya
Ligi Kuu.
Mwamuzi Ludovic Charles
amepewa onyo kali kwa kutodhibiti vizuri mchezo. Uamuzi dhidi yake ni
kwa mujibu w Kanuni ya 38(5) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.
No comments:
Post a Comment