Kada
wa Chadema Yeriko Nyerere, amekamatwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni
polisi au usalama wa taifa leo akiwa nyumbani kwake Kigamboni, Mbutu.
Taarifa
iliyotolewa na Meya wa Ubungo, Boniphace Jacob imeeleza kuwa Nyerere
alikamatwa na watu hao ambao waliambatana na Mwenyekiti wa Kijiji cha
Mbutu.
“Nimepata
taarifa kutoka kwa ndugu wa Yeriko ambao wamenipigia simu alfajiri leo.
Wamesema amekamatwa saa tisa usiku na watu hao ambao walivalia kiraia.
Viongozi wa Chadema wanaelekea polisi kufuatilia kwa kina chanzo cha
Yeriko kukamatwa,” amesema Jacob
No comments:
Post a Comment