Mbunge
wa Kigoma Mjini, Zuberi Zitto Kabwe amesikitishwa na kitendo
kilichofanywa na moja ya askari polisi kumtishia bunduki aliyewahi kuwa
Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima.Zitto kabwe ameonyesha masikitiko hayo
kupitia ukurasa wake wa kijamii Facebook akihoji kama polisi wanafundishwa
kuwafanyia hivyo raia.Hii ni nini ?, askari wetu wanafundishwa kufanya
hivi, Waziri Mwigulu huyu yupo wazi na ni wa kutoka kwako. Unahitaji
uchunguzi". Ameandika Zitto
Zitto
ameandika hayo baada ya masaa machache kupita kwa tukio hilo
lililowahusisha askari hao walioambatana na kampuni ya Majembe Auction
Mart waliokuwa wakitaka kujaribu kukamata gari iliyokuwa imeegeshwa
pembeni ya barabara ya Masaki karibu na Hoteli ya Double tree ingawa
ndani ya gari hilo alikuwepo dereva.
No comments:
Post a Comment