Baadhi
ya wadau akiwemo msanii mkongwe wa muziki nchini kutoka Morogoro,
Afande Sele ameonyesha kutoridhishwa na zawadi ya gari aliyopewa Miss
Tanzania 2016/17, Diana Edward kwa madai limechakaa na linashusha hadhi
ya mashindano hayo nchini.
Rapa huyo ameishauri wizara husika kubadili jina la shindano hilo kwa madai wanalitia aibu Taifa.
“Utapeli
ni nini?. Gari ya Miss Tanzania 2017 na gari ya Miss Tanzania 2011
zinatoa jibu la swali hilo,” aliandika Afande Sele Intagram. “Lakini pia
ni vyema tukamuomba waziri husika katika masuala hayo akamuulize
muandaaji wa Miss Tanzania kama ni kweli ameamua kuzeeka labda hata kufa
na shindano lake?,”
Aliongeza,
“Na kama kweli iko hivyo basi itoshe pia kubadili jina la shindano kwa
kuliita miss jina lake badala ya kuendelea kutia aibu faifa kwa kuliita
Miss Tanzania huku likikosa hadhi ya kitaifa katika maeneo yote kwa
makusudi na maslahi yake yeye mtu mmoja tu. Aibu yake aibu yetu.
Imetosha sasa, imetosha sana,”
Miss huyo alikabidhiwa gari hilo wiki iliyopita baada ya kusubiri kwa zaidi ya miezi sita
No comments:
Post a Comment