Wanamuziki
wakali wa Bongo fleva kama Diamond, Ali kiba, Vanessa Mdee na Darassa
wameng’aa kimataifa zaidi baada ya kila mmoja kujishindia tuzo za Hippo
nchini Uganda.
Tuzo
hizo zilifanyika usiku wa jana nchini Uganda ambapo baadhi ya wasanii
waliopata Tuzo kutoka Tanzania ni kama vile Diamond, Ali Kiba, Vanessa
Mdee na Darassa.
Vanessa
Mdee ameibuka na tuzo ya heshima katika kipengele cha ‘East Africa Best
Female Artist’ na Alikiba akiibuka na tuzo ya kipengele cha ‘Song of
the Year Tanzania’ kupitia wimbo wake wa Seduce Me.
Diamond
Platnumz ameshinda tuzo mbili mbili kwenye vipengele vya ‘Africa Song
of The Year’ kupitia wimbo wake wa ‘Marry U’ aliomshirikisha Ne-Yo na
‘Best East Africa Video’ kupitia wimbo wa Eneka.
Darassa ameibuka kidedea kwenye kipengele cha ‘East African Super Hit’ na wimbo wake wa Muziki ambao amemshirikisha Ben Pol.
No comments:
Post a Comment