KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

March 19, 2018

VIGOGO TPDC WAMEKABIDHI HATI ZA KUSAFIRIA MAHAKAMANI

Vigogo watano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) wanaokabiliwa na shtaka la matumizi mabaya ya madaraka, leo Machi 19, 2018  wamewasilisha hati zao za kusafiria katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Hati hizo zimewasilishwa mbele ya hakimu mkazi mkuu, Wilbard Mashauri huku upande wa mashtaka ukiwakilishwa na wakili wa Serikali, Emmanuel Jacob.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 18, 2018 kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa wanaokabiliwa na kesi hiyo ni aliyekuwa mkurugenzi mtendaji, James Mataragio,  kaimu meneja wa uvumbuzi, George Seni, mkuu wa kitengo cha ununuzi na utawala, Wellington Hudson, mkurugenzi wa mkondo wa juu, Kelvin Komba na Edwin Riwa ambaye ni kaimu mkurugenzi wa mipango.

No comments:

Post a Comment