Katibu
Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Godfrey Mngereza amesema
mwanamuziki Nassib Abdul maarufu Diamond amefanya makosa kumjibu Naibu
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza
akifananisha kitendo hicho na kuitukana Serikali.
Diamond
Platnumz na naibu waziri huyo waliingia katika vita ya maneno baada ya
Serikali kufungia nyimbo 15 mwezi uliopita, zikiwemo mbili za
mwanamuziki huyo.
Mngereza
amesema Diamond anapaswa kuelewa kwamba maneno machafu anayoyatoa dhidi
ya waziri huyo ni sawa na kuitusi serikali jambo ambalo hata ukienda
katika sheria za kimtandao anaweza kujikuta anaingia matatizoni.
Mngereza
amesema wamesikitishwa na kauli ya Diamond na kusisitiza kwamba ni
vyema akafuata taratibu katika kulalamikia suala hilo ikiwemo kuandika
barua kama alivyomuelekeza Waziri Shonza.
Ameongeza
kuwa si lazima msanii aandikiwe barua pale anapokosa kama ambavyo
Diamond ameeleza katika ukurasa wake wa Twitter, kwamba Shonza
angemwandikia barua kabla ya kumfungia.
Amebainisha kuwa si kila mwanamuziki anayefanya makosa huwa anaandikiwa barua.
Katika
malalamiko yake, Diamond amesema naibu waziri huyo amekuwa akikurupuka
kufungia nyimbo na pia kutowaandikia barua rasmi ndio maana ameamua
kuyazungumza kwenye redio na mitandao ya kijamii.
Jana
Waziri Shonza alisema hawezi kujibizana na Diamond kwa sababu
alichofanya si maamuzi yake binafsi na kwamba kama anaona ameonewa
apeleke malalamiko yake kwa maandishi.
No comments:
Post a Comment