Wakati
BASATA wakimtuhumu Diamond kulewa na umaarufu na kufanya abishae na
Naibu waziri ambaye anawakilisha Serikali, bado huko katika mitandao ya
kijamii watu wamezidi kuonyesha hisia zao juu ya jambo hilo kwa kudai
kuwa Naibu waziri anatafuta kiki kwa lengo la Kumshusha Diamond.
Mwanahabari
na Blogger, Le Mutuz ameibuka na kudai kwa Naibu Waziri amekuwa
akitumiwa na watu wenye chuki kubwa na muziki wa Diamond ili kuua muziki
wake na sio vinginevyo.
Le
Mutuz anasema kuwa huu ulikuwa ni wakati wa serikali kuona mchango wa
Diamond hasa baada ya kuchaguliwa kwenda kufanya show ya ufumbuzi wa
kombe la
Dunia.
Lemutuz
ambaye amesema kuwa pamoja na kwamba Mh Juliana Shonza ni mwana CCM
mwenzake lakini anaona kabis katika hili la kuwafungia na kubishana na
Diamond katika mitandao ya kijamii hawezi kunyamaza kimya.
Hata
hivyo Lemutuz amemhusisha Julana Shonza na moja ya kiongozi wa kituo
fulani cha radio “MUNGU MTU” ambacho hajakitaja na kusema kuwa wamekuwa
wakishirikiana ili kumtua Diamond katika nafasi kubwa ya mafanikio ya
kimuziki aliyonayo.
No comments:
Post a Comment