Mwenyekiti
wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo amesafirishwa
usiku wa kuamkia leo Machi 21, 2018 kupelekwa mkoani Iringa.
Taarifa
zilizotolewa na wakili wake, Jebra Kambole leo Jumatano Machi 21, 2018
zinaeleza kuwa sasa Nondo yupo Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa.
Nondo
anadaiwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha Machi 6, 2018 na siku
inayofuata akaonekana mjini Mafinga, wilayani Mufindi, Iringa ambako
alishikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo na baadaye kurejeshwa Dar es
Salaam.
Tangu
akamatwe Nondo hajawahi kuzungumza na wakili wake wala mtu yeyote wa
karibu yake jambo ambalo limekuwa likipingwa na watetezi wa haki za
binadamu.
Jana,
Jebra alisema kuwa wamefungua kesi kwa ajili ya kuiomba mahakama mambo
matatu, kwanza kumpa dhamana Nondo, pili kutoa amri ya kuwapa mawakili
haki ya kuonana na Nondo na kingine ni kuitaka mahakama itamke
mwanafunzi huyo wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) ameshikiliwa kinyume
cha sheria.
No comments:
Post a Comment