Mbunge
wa Nzega (CCM), Hussein Bashe amewahakikishia wananchi wa Tanzania kuwa
hoja yake aliyoiwakilisha kwa Katibu wa Bunge kuwa haiwezi kukwamishwa
na jambo lolote kwa madai hakuna kisichojulikana kinachoendelea kutoka
katika nchi.
Bashe
ametoa kauli hiyo leo (Machi 08, 2018) wakati alipokuwa anazungumza na
waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuelezea sababu
zilizompelekea yeye kama Mbunge kuandika barua ya kutaka kuundwe kwa
kamati ya uchunguzi dhidi ya matukio mbalimbali yanayoonesha kutishia
umoja, usalama na mshikamano wa taifa la Tanzania.
"Madhumuni
ya kikatiba ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ni kuwasemea wananchi,
kuwatetea kwa hiyo natimiza wajibu wangu kama Mbunge sioni kama
nitapoteza Ubunge wangu katika hili.
"Mimi
ninaamini nitapoteza ubunge wangu kwasababu zifuatazo, endapo
nitashindwa kutimiza wajibu wangu ndani ya Bunge, nikishindwa kutimiza
wajibu wangu ndani ya Jimbo langu kwa maana nimeshindwa kuisimamia
serikali katika kuleta maendeleo, nimeshindwa kutimiza ahadi wakati wa
uchaguzi katika jimbo langu na mwisho wanaccm watakaposema kwenye
mchakato wa kidemokrasia wa kura kwamba Hussein wewe hapana.
"Mimi
ni muumini wa kiislamu ninaamini kila binadamu umauti utamfika (kifo)
na chochote kitakachonifika ni kile ambacho amekipanga Mwenyezi Mungu
lakini sina hofu yeyote kwasababu hili sio taifa la namna hiyo.
"Nikiwa
kama Hussein sidhani hii hoja kama inakwenda kukwama kwasababu
unapoikwamisha hoja unapaswa kusema unaikwamisha kwa kutumia misingi
gani kama watu wanaamini kwa kila kinachotokea ndani ya ardhi ya
Tanzania sioni kama itakwama.
"Bunge
limeshafanya maamuzi mbalimbali juu ya masuala mbalimbali katika rekodi
ya nchi hii, kwa hiyo mimi nadhani ni muhimu tukatoa fursa jambo hili
lifike Bungeni na likifika huko kama litakataliwa basi tujue ni
kwasababu zipi na kama nilivyofanya kuwaambia watanzania ndivyo hivyo
nitarudi kuwaambia limekataliwa kwasababu zipi na hapo tutajadili hatua
za kufanya".
Kwa
upande mwingine, Bashe amesema anasubiria majibu ya barua aliyotuma
kutoka kwa Katibu wa Bunge Pamoja na Katibu Chama cha Mapinduzi (CCM)
ambayo ameeleza dhamira na nia yake huku akisisitiza zaidi kuwa jambo
hilo hajalifanya kwa mihemuko (kukurupuka) bali amefanya kwa umakini wa
hali ya juu na utafiti wa kutosha.
No comments:
Post a Comment