Hayo
yameelezwa leo Machi 8 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri na
wakili anayewatetea, Evodius Mtawala wakati kesi hiyo ilipotajwa
mahakamani hapo.
“Mshtakiwa
wa kwanza Aveva, tangu jana amelazwa katika kitengo cha wagonjwa
mahututi hali yake siyo nzuri," ameeleza wakili Mtawala.
Hata
hivyo, mwendesha mashtaka wa Takukuru, Leonard Swai naye ameliambia
mahakama kuwa Aveva ni mgonjwa na kwamba upelelezi wa kesi hiyo bado
haujakamilika.
Baada
ya kutolewa kwa maelezo hayo, Mtawala ameiambia mahakama kuwa
walizungumza na upande wa mashtaka wataeleza jalada la kesi hiyo bado
lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na wameomba wapewe siku 14 ili
waweze kueleza kitu.
Hakimu Mashauri ameiahirisha kesi hiyo hadi Machi 22, 2018.
Wakati kesi hiyo ikitajwa mahakamani hapo alikuwapo Godfrey Nyange maarufu Kaburu ambaye ni makamu wa rais wa Klabu ya Simba.
Washtakiwa
hao wanakabiliwa na mashtaka matano ya uhujumu uchumi ikiwamo
kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha wa kiasi hicho cha
fedha.
Washtakiwa
hao wapo mahabusu kutokana na kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji
fedha ambayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.
No comments:
Post a Comment