Mfuasi
wa CHADEMA, Ally Rajabu anayekabiliwa na kesi ya kufanya mkusanyiko
usio halali ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa anaomba
arejeshewe gari lake ambalo lipo mikononi mwa polisi.
Ally
Rajabu ni mshtakiwa wa 28 kati ya 31 wakiwemo watatu waliopigwa risasi
na Polisi ambao ni wafuasi wa chama hicho wanaokabiliwa na kesi ya
kufanya mkusanyiko usio halali maeneo ya Kinondoni Mkwajuni Dar es
Salaam.
Awali
kabla ya kueleza hayo, Wakili wa Serikali Aldo Mkini, amemueleza Hakimu
Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa upelelezi wa shauri hilo bado
haujakamilika.
Naye Wakili wa utetezi, Alex Massaba amedai kuwa wateja wake wawili ni wagonjwa na wameshindwa kufika mahakamani hapo.
Baada
ya kueleza hayo, mshtakiwa wa 28, Ally Rajabu ameieleza mahakama kuwa
anaomba kurudishiwa gari lake ambalo linashikiriwa na Jeshi la Polisi
tangu siku ya maandamano.
Hata
hivyo, Hakimu Mashauri amesema kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa
kuingilia masuala yaliyofanyika Polisi ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi
April 4, 2018.
Washtakiwa
wengine katika kesi hiyo ni Thabitha Mkude, Khaji Lukwambe, Emmanuel
Kimio, Mohamed Juma, Husein Mnimbo na wenzao kwa pamoja wanadaiwa kati
ya February 16, 2018 maeneo ya Mkwajuni Kinondoni DSM walifanya
mkusanyiko usio wa halali kinyume cha sheria.
No comments:
Post a Comment