Serikali
ya Nigeria imethibitisha kuwa wengi kati ya wanafunzi wa kike 110
waliokuwa wametekwa na kikundi cha Boko Haram zaidi ya mwezi mmoja
uliopita wameachiwa Jumatano asubuhi.
Shirika
la habari la AFP limeripoti kuwa wasichana hao waliletwa katika mji wa
Dapchi ulioko upande wa Kaskazini mwa Nigeria wa Jimbo la Yobe baada ya
wale waliokuwa wanawashikilia kuwarejesha katika msafara ulioandamana na
magari 9.
Ripoti
za vyombo vya habari zimesema wasichana watano kati ya hao walikufa
wakati wakisafirishwa, lakini afisa wa serikali wa jimbo la Yobe amesema
hili bado halijaweza kuthibitishwa.
Waziri
wa Habari wa Nigeria Lai Mohammed amesema kuachiwa kwa wasichana hao
mapema asubuhi “bila masharti” kulitokana na “juhudi za kisiri”
zikisaidiwa na “baadhi ya marafiki wa nchi hiyo.”
“Wasichana 91 na mvulana mmoja wameelezewa kuwa wameachiwa. Hayo ndio yaliyojiri,” amewaabia waandishi.
“Wengi
kati ya wasichana hao, wengi wa wanafunzi hao walioachiwa huru
hawakuletwa wote sehemu moja. Waliachwa njiani na wao wenyewe walirudi
majumbani kwa wazazi wao.
Vyanzo vya habari nchini Nigeria vimetoa habari kuwa wakazi wa eneo la Dapchi walikuwa wanafurahia kuachiwa kwa watoto hao.
Wazazi ambao hapo awali walikuwa wanamsiba kwa kutekwa kwa vijana wao hivi sasa wanasheherekea kurudi kwao.
No comments:
Post a Comment