Watu
saba wamefariki dunia katika ajali ya gari aina ya Scania iliyotokea
katika Kijiji cha Mkongoro, Barabara ya Manyovu Wilaya ya Kigoma
Vijijini.
Kamanda
wa Polisi mkoani Kigoma, Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kuongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva kushindwa kuimudu
gari kwenye mteremko.
Amesema
ajali hiyo imetokea jana Jumatano Machi 21, saa tatu asubuhi katika
Mlima wa Kasagamba ambapo lori lenye namba T741AAB lilianguka na
kusababisha vifo vya watu saba akiwamo dereva wa gari hiyo aliyefahamika
kwa jina la Siri Hamis (43) mkazi wa Singida pamoja na utingo wake
aliyefahamika kama Ramadhani Saidi (23).
“Katika
gari hiyo walikuwa wamebeba mizigo na watu wanne mmoja mwanamke na
watatu wanamume ambapo wengine waliofariki na majina yao hayakufahamika
mara moja.
“Ajali
hiyo pia imesababisha kifo cha mwanafunzi aliyefahamika kwa jina la
Eliakimu Samsoni (15 ), aliyekuwa akitembea kwa miguu kuelekea shuleni
na gari hilo kumgonga akiwa anatembea,” amesema Kamanda Otieno.
No comments:
Post a Comment