Mbunge
wa Jimbo la Hanang, mkoani Manyara Dkt Mary Nagu (CCM) na mwenyekiti wa
CCM wilaya hiyo jana walikamatwa na Jeshi la Polisi wilayani humo kwa
amri ya Mkuu wa wilaya hiyo kutokana na sababu ya kushindwa kuelewana
kiutendaji.
Kwa
mujibu wa mkuu wa wilaya Sarah Msafiri ameeleza kuwa aliagiza kukamatwa
kwa Mbunge huyo baada ya kuchoka kumvumilia kutokana na kauli
anazozitoa kwenye mikutano yake na wananchi akihamasisha wasishiriki
shughuli za maendeleo.
Pia
amemtuhumu Mbunge huyo kuwataka wananchi wasishirikiane naye jambo
ambalo alidai ni sawa na kuwataka wananchi wasishirikiane na serikali
kwa sababu yeye anasimama kama serikali
“Ni
kweli tumemkamata na sababu kubwa ni kuhamasisha wananchi wasishiriki
shughuli za maendeleo na pia anawataka wananchi wasishirikiane na Mimi
wakati anajua Mimi nasimama kama serikali” -DC Msafiri
No comments:
Post a Comment