Mwenyekiti
wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania , Abdul Nondo ambaye pia ni Mwanafunzi
wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) aliyeripotiwa kupotea katika
mazingira ya kutatanisha amepatikana akiwa hai eneo la Mafinga mkoani
Iringa.
Imeelezwa
kuwa, Nondo alijikuta katika eneo hilo baada ya kuzinduka kutoka katika
lindi la usingizi na kuwauliza wenyeji wa eneo hilo kuwa hapo ni wapi?
Wenyeji hao walimfahamisha kuwa yuko Mafinga mkoani Iringa na kisha
akapelekwa katika kituo cha polisi kilichoko karibu.
Polisi walifanya mahojiano na mwanafunzi huyo ili kuweza kujua nini hasa kilitoka na baada ya hapo kupiga simu kwa ndugu zake.
Baada
ya Baba mzazi, Mussa Mitumba kupata taarifa za kuonekana kwa mwanae,
aliomba namba za askari aliyemfanyia mahojiano ili kujua nini kilimpata
mwanae aweze kujua kama jambo jingine alilowaambia kuhusiana na kupotea
kwake.
Awali kabla ya tukio hilo mwanafunzi huyo alielezea kwamba alikuwa akifuatiliwa mara kadhaa watu asiowatambua
No comments:
Post a Comment