Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
jana amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) Bw. Li
Yong.
Katika mkutano huo ambao ulikuwa na lengo ya kujadiliana masuala mbalimbali ya uendelezaji Viwanda nchini Tanzania.
Mkurugenzi huyo amemjulisha Makamu wa Rais kuwa Tanzania ni nchi ya nne kuitembelea tangia ateuliwe .
Aidha
katika mazungumzo hayo Mkurugenzi wa UNIDO amesema anajua Tanzania
ajenda yao kuu ni uanzishwaji wa Viwanda na alimhakikishia Makamu wa
Rais kwamba UNIDO itajitahidi kusaidia ajenda hiyo.
“Kuna
umuhimu wa kuzingatia sekta binafsi na viwanda vidogo na vya kati
wakati wa uanzishwaji viwanda ili vijana na wanawake wapate ajira,”
alisema Mkurungenzi Mkuu wa UNIDO.
Mkurugenzi
Mkuu wa UNIDO Bw. Li Yong amesema pia suala la uanzishwaji na
Uendelezaji wa Viwanda ni lazima lizingatie masuala ya upatikanaji wa
nishati na mabadiliko ya tabia nchi.
Aidha
Mkurugenzi huyo alisifia mabadiliko ya kiuchumi na kijamii
yanayoendelea ndani ya Serikali ya awamu ya tano na kusema UNIDO suala
muhimu ni Utekelezaji.
Pia aliupongeza uongozi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania na mashirikiano mazuri na Serikali.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
alimhakikishia Mkurungenzi huyo wa UNIDO ushirikiano wa hali ya juu
kutoka Serikalini na alimuomba kuipa Tanzania kipaumbele katika
programu yake muhimu itakayochochea maendeleo ya Viwanda ya “Programmes
For Country Partnership-PCP”.
Mwisho Kiongozi huyo aliishukuru Tanzania kwa mapokezi mazuri na programu nzuri walizompangia.
Viongozi
wengine walioshiriki kwenye mazungumzo hayo ni Waziri wa Viwanda,
Bishara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage, Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Philip Mgango pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Mhe. Balozi Augustine Mahiga ambapo pia Waziri wa
Viwanda , Biashara na Uwekezaji alitia saini pamoja na Mkurugenzi Mkuu
wa UNIDO Bw. Li Yong
Tamko
la Kusudio la kuanzisha (Declaration of Intention) Mpango wa UNIDO
unaojulikana kama “Programmes For Country Partnership-PCP” ambapo
Makamu wa Rais alishuhudia kusainiwa kwa Tamko hilo,kusainiwa kwa tamko
hilo kutarahisisha mchakato wa wa kukamilika kwa uwasilishwaji wa ombi
la Tanzania kuomba iingizwe katika Mpango Maalumu wa UNIDO ambao ni
muhimu katika kuchochea maendeleo ya Viwanda.
No comments:
Post a Comment