Akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu masuala ya maendeleo endelevu ya Wanawake barani Afrika, Prof. Ndalichako amewataka wanawake kufanya kazi kwa bidi ili waweze kuaminiwa na jamii.
“Wito wangu ni kwamba tuendelee kufanya kazi kwa bidii kwa sababu historia imemuweka mwanamke katika nafasi isiyo nzuri kwa hiyo wanawake tukiendelea kufanya kazi kwa bidii mchango wetu kwa jamii utaendelea kuonekana na kuthaminiwa na hivyo tunaweza tukawa tunapata nafasi kubwa na nzuri ya kulitumikia taifa, hii historia ya kubaki nyuma tutaiondoa wanawake wenyewe kwa kufanya kazi kwa bidi,” amesema.
Naye Makinda amewataka wanawake kujiamini sambamba na kuwa na uthubutu huku akiwasihi kujitika katika utafutaji wa elimu kwani ndiyo mkombozi wa maendeleo ya wanawake.
“Elimu ni kitu muhimu sana, wanawake wengi elimu zao ni ndogo wananyanyasika wananyang’anywa mali sababu hawajui wanaenda wapi, elimu yenyewe siyo ya utaniutani, wenyewe wanasoma lakini hawajui wanasoma nini. Mkombozi wa mwanamke ni kupatikana elimu sahihi ya kuweza kupambanua maisha yake na kujua haki zake ziko wapi na si kumdekeza sababu ukimdekeza hatuwezi kufanya chochote,” amesema na kuongeza.
“Elimu inamfanya mwanamke athubutu, kama huna elimu hijuamini ndiyo unatengeneza mazingira ya kupata mafanikio kwa kupitia mtu, kusoma vizuri kujiamini, kuwa na uthubutu mwengine anataka kwenye kazi apelekwe na mtu.”
Na Regina Mkonde
No comments:
Post a Comment