Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, ametangaza mpango kabambe wa
kuviwezesha vikundi vya mazoezi ya kukimbia (jogging club) kwa kuweka
utaratibu wa mashindano ya kila mwisho wa mwezi.
Ambapo kikundi kitakachoshinda kitapatiwa kiasi cha shilingi milioni 10 kama mtaji wa kufanya shughuli za kujikwamua kiuchumi.
Hatua
hiyo imekuja baada ya Makonda kubaini idadi kubwa ya vijana hao
wakimaliza mazoezi asubuhi hawana shughuli ya kufanya hivyo wanakaa
vijiweni.
”Vijana
wengi wa ‘Jogging Club’ hizo wanafanya mazoezi asubuhi halafu hawana
kazi za kufanya wanarudi vijiweni, hiyo si salama maana unaweza
ukashangaa wakajikuta wameanza kuwa na ‘speed’ kubwa na matokeo yake
wakapita na mikoba ya wakina mama kama hawana kazi za kufanya.
Ameongezea
”Kwa hiyo sisi tunaratibu na kupitia hadhara hii niwaambie wananchi
kwamba tunapanga mipango kwa kila mwisho wa mwezi kuwepo na mashindano
‘Jogging Club”, amesema Makonda.
Amesema
kitendo cha kukaa kijiweni kinaweza kuwasababishia kushawishika kufanya
vitendo vya uhalifu hivyo kwa kuwapatia mtaji itawawezesha kufanya
shughuli za uzalishaji mali utakaowakwamua kiuchumi.
Amesema
mashindano hayo yataanza rasmi mwezi ujao, na kwa kuanzia shindano hilo
litaanzia wilaya ya Temeke kwa kuwa ndiyo inayoongoza kwa Jogging Club,
kwa Dar es salaam, hivyo amezitaka jogging club zote za mkoa kukutana
Temeke.
No comments:
Post a Comment