Kufuatia
Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi “East Africa
Crude Oil Pipeline (EACOP)” kutoka Hoima nchini Uganda hadi
Chongoleani, Tanga nchini Tanzania, Taesa imetoa ufafanuzi namna ya
kujisajili na ajira hiyo ili kuweza kutambulika.
Mradi
huo ambao ujenzi wake unatarajiwa kuchukua kati ya miezi 24 hadi 36,
unategemewa kuzalisha fursa za ajira takribani 10,000 wakati wa ujenzi
na ajira zaidi ya 1,000 wakati wa uendeshaji wake.
Hivyo
Watanzania wote wenye taaluma na ujuzi katika Sekta ya Mafuta na Gesi
wanatakiwa kujisajili TaESA kwa kuingiza taarifa zao lengo likiwa
kuiwezesha Serikali kubaini idadi halisi ya Watanzania walio na sifa
zinazohitajika na walio tayari kuajiriwa kwenye mradi huo.
Zoezi
la usajili limekwishaanza na linatarajiwa kukamilika tarehe 30/03/2018,
na usajili unafanyika kwa kujaza fomu maalumu inayopatikana katika
tovuti ya www.taesa.go.tz, au kwa kufika kwenye ofisi zao za kanda zilizoko Dar es Salaam, Arusha, Dodoma na Mwanza.
Fomu zilizojazwa zinaweza kuwasilishwa kwenye ofisi zao za kanda au kwa barua pepe: eacop@taesa.go.tz. Kwa maelezo zaidi wasaliana nao kupitia namba zifuatazo: 0736 551 055; 0739 221 022; 0735 221 022; 0735 551 055 na 0282 541 840/1.
Mradi
huu ni moja ya miradi mikubwa kutekelezwa nchini, unaotegemea kugharimu
Dola za kimarekani 3.5 sawa na bilioni 8 za kitanzania
Bomba hilo litakuwa na urefu wa wa kilometa 1,445 ambapo ujenzi wa kilometa 1,115 za bomba hilo utafanyika nchini Tanzania.
Jumla ya wilaya 24 na vijiji 184 hapa nchini vinategemewa kupitiwa na bomba hilo katika mikoa 8 ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga.
Bomba hilo litakuwa na urefu wa wa kilometa 1,445 ambapo ujenzi wa kilometa 1,115 za bomba hilo utafanyika nchini Tanzania.
Jumla ya wilaya 24 na vijiji 184 hapa nchini vinategemewa kupitiwa na bomba hilo katika mikoa 8 ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga.
No comments:
Post a Comment