Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imepokea msaada wa vitanda 14, magodoro
12 pamoja na drip stands kutoka Australia Tanzania Society ambavyo
vitasaida kuimarisha utoaji wa huduma hospitalini hapo.
Akipokea
msada huo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa
MNH, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Dkt. Juliethi Magandi amesema kwa
muda mrefu hospitali imekua na ushirikiano na tasisi hiyo katika
masuala mbalimbali ikiwemo kufanya upasuaji wa ubingwa wa juu.
“Kipekee
nichukue fursa hii kuwashukuru rafiki zetu hawa Australia Tanzania
Society kwa msaada huu walioutoa kwani tumekua tukishirikiana kwa zaidi
ya miaka mitatu sasa,”. amesema Dkt. Magandi.
Amesema
Hospitali ya Taifa Muhimbili ina jumla ya vitanda 1,507 na kwamba kina
mama wajawazito na watoto pekee wanatumia karibu ya nusu ya vitanda
hivyo. “Hivyo msaada huo umekuja wakati muafaka kwani hospitali bado
ina mahitaji kutokana na kutoa huduma zake kila siku kwa saa 24,”.
“Kati
ya vitanda hivi 14 tulivyopewa leo, sita tumevileta wodi 35 kwa ajili
ya kina mama na vingine 8 tumepeleka ICU namba moja na ICU namba mbili’’
amefafanua Dkt. Magandi.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society, James Chialo
amesema msaada huo umegharimu zaidi ya shilingi milioni 25 na kwamba
lengo ni kuboresha huduma za afya hususani katika hospitali za Umma.
“Kutoa
ni moyo si utajiri tutaendelea kushirikiana katika kuboresha huduma za
afya kadiri hali inavyoruhusu nitoe wito kwa wadau wengine kuendelea
kushirikiana ili tuboreshe huduma za afya nchini ‘’amesema Bwana Chialo.
Mkurugenzi
wa Huduma za Upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt.
Julieth Magandi akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kabla
kukabidhiwa vitanda 14 na magodoro 12 ambayo yametolewa na Australia
Tanzania Society. Kulia ni Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society,
James Chialo na kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uuguzi na Mazingira
Muhimbili, Zuhura Mawona.
Muuguzi
Alice Msonda na Velena Joahackim wakitandika kitanda baada ya
kukabidhiwa vitanda na magodoro na Australia Tanzania Society.
Mkurugenzi
wa Australia Tanzania Society, James Chialo akimkabidhi Mkurugenzi wa
Huduma za Upasuaji wa Muhimbili, Dkt. Julieth Magandi vitanda 14 leo.
Katikati ni Mkuu wa Idara ya Uuguzi na Mazingira Muhimbili, Zuhura
Mawona.
Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society, James Chialo akizungumza na waandishi wa habari leo kabla ya kukabidhi vitanda hivyo.
No comments:
Post a Comment