Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amesema mapambano ya magonjwa yasiyoambukiza
yatafanikiwa endapo sekta nyingine mbali na afya zitashirikishwa.
Majaliwa
ameyazungumza hayo jana wakati akifungua mkutano wa 65 wa mawaziri wa
afya wa Jumuiya za nchi za Mashariki, Kati na Kusini mwa bara la Afrika
uliowashirikisha mawaziri kutoka nchi tisa.
Alisema
kutokana na ongezeko la magonjwa hayo, nchi hizo zinapaswa kuangalia
namna ambavyo zitatatua ongezeko hilo ili kupunguza gharama.
"Ili
kuepuka kutumia gharama kubwa katika kutibu magonjwa haya juhudi za
makusudi zinapaswa kuchukuliwa ikiwemo kushirikisha sekta nyingine
katika kutatua changamoto zilizopo lakini zaidi ni kuelimisha jamii
kubadili mfumo wa maisha," alisema Majaliwa.
Mwakilishi
kutoka Benki ya Dunia (WB), Dk Paolo Belli alisema nchi hizo kwa sasa
zinatakiwa kutumia teknolojia mpya ili kupata matokeo mapya katika
magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa yasiyoambukiza, TB na vifo vya
wajawazito na watoto.
Aidha,
amezishauri nchi hizo kuangalia uwezekano wa kupunguza matumizi ya
tumbaku kwa kuwa yanasababisha madhara kwa watu wengi ikiwemo gharama
za kutibu magonjwa mengi yatokanayo na madhara ya tumbaku.
No comments:
Post a Comment