Mahakama
Kuu nchini imetoa wito wa kuwaita DCI, IGP na AG kufika mahakamani
siku ya Jumatano ya tarehe 21 kujibu kesi ya kutomfikisha mahakamani
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP) Abdul Nondo.
Taarifa za wito huo zimetolewa na Wakili wa Mwanafunzi huyo wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Wakili Jebra Kambole.
Kambole amesema "Wito
umetolewa Mahakama kuu mbele ya Jaji Rehema Sameji. kwamba DCI, IGP na
AG wanapaswa kufika mahakamani 21/03/2018 kujibu kesi ya Abdul Nondo".
Kambole
amesema washitakiwa katika kesi hiyo itakayosikilizwa Jumatano ni ;
IGP Sirro ambaye ameitwa kwasababu yeye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini hivyo vituo vyote na polisi wapo chini yake lakini bado Nondo
amekuwa hapatikani katika vituo vya polisi.
Aidha
Kambole amesema kuwa katika jalada lililofunguliwa, Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), naye kahusishwa kwa sababu mara ya
mwisho Nondo alipokelewa na yeye alipofikishwa Dar es salaam kutoka
Iringa na kwamba alimchukua kama muathirika wa tukio la utekwaji na siyo
mshtakiwa.
Hata
hivyo Kambole amesema ameshafanya jitihada nyingi za kutaka kuonana na
mteja wake lakini hadi sasa juhudi zake hazijafua dafu.
Abdul
Nondo anashikiliwa na jeshi la polisi tanguMachi 7, ambapo awali
aliripotiwa kupotea kusikojulikana na kesho yake kujikuta Iringa, ambapo
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Lazaro Mambosasa amesema mpaka sasa
wanamshikilia Nondo kwa ajilili ya upelelezi na watakapokamilisha
watamfikisha mahakamani.
No comments:
Post a Comment