Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amesema amemuagiza na
kumuelekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro kuwakamata
watu wote ambao wamepanga njama za kutaka kuwauwa watanzania katika
maandamano ambayo wameyapanga kuyafanya
Mwigulu
ametoa hiyo wakati alipokuwa akitoa salamu zake kwa Rais Dkt. Magufuli
aliyopo Mkoani Singida katika ziara yake ya kikazi ambapo leo hii (Machi
11, 2018) amezindua kiwanda cha Alizeti Mkoani humo na kusema
kinachotafutwa katika maandamano hayo ni namna ya watu wanatawanywa ili
kusudi waje kulalamika kuwa serikali ndio imeuwa watu wake.
"Njama
hiyo tumeiona na mimi nimemuelekeza IGP Sirro kwamba hata kupanga njama
ya kuua ni kosa, wachukue hatua kwa wale watu wanaopanga mipango ya
aina hiyo na kuchafua taswira ya nchi yetu ama kwa mipango yao au ya
wale wanaowatuma.
"Watu
wanataka mikusanyiko ili wafyatue na kuuwa watu ili kuchafua taswira
ya nchi yetu na tunayo mifano wa maeneo waliwahi kufanya jambo la aina
hiyo na hatua zitachukuliwa", amesema Mwigulu.
Pamoja
na hayo, Mwigulu ameendelea kwa kusema "Mhe. Rais ndio maana unaona
vinyago vinyago vingi hivi kama hivi juzi alitokea kijana mdogo amesema
ametekwa, eti ametekwa na akapata muda wa kutafuta pafyumu na nguo za
kubadilishia kule atakapokuwa ametekwa.
"Unatowa
wapi muda wa kujiandaa ?, watu wanatafuta njia za kuchafua taswira ya
nchi yetu, na jambo hili Mhe. Rais kama ambavyo ulishatoa maelekezo, si
jambo ambalo tutacheza nalo wala mjadala, hakuna sababu ya maandamano
wala hakuna sehemu ya kuandamania na hakuna ruhusa ya kuandamana".
Aidha,
Waziri Mwigulu amesema endapo ikatokea hata watu wakaandamana ndani ya
nyumba zao bado sheria itachukua mkondo wake dhidi ya watu hao.
"Ikitokea
hata watu wakaandamana ndani ya nyumba wakazunguka kitanda na akatokea
mtu akaumia, yule aliyeitisha waandamane pale atawajibika kwasababu watu
wanafanya mzaha na maisha na dira ya nchi yetu ambapo Rais umejitoa
muhanga kwa ajili ya kutengeneza urithi wa watoto wa Tanzania",
amesisitiza Mwigulu.
Kwa
upande mwingine, Waziri Mwigulu amesema yeyote atakayethubutu kutaka
kuharibu taifa la Tanzania kwa kufanya vitendo vya uovu hawatoweza
kumuacha salama.
No comments:
Post a Comment