Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Mh. Paul Makonda amefunguka na kuwaomba
msamaha baadhi ya wananchi ambao ameshindwa kutimiza ndoto zake na
kusema anaamini ataendelea kuwatumikia na kujitahidi kuweza kugusa
maisha ya kila mmoja.
Paul
Makonda amesema hayo siku mbili baada ya kutimiza miaka miwili toka
ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kusema kuwa ndani ya
miaka miwili akiwepo madarakani anaamini amegusa maisha ya watu kwa
kutumia kipaji chake, uwezo wake wote.
"Asante
Mungu kwa neema zako, kama usingekuwa upande wangu na Dunia iseme sasa.
Nawashukuru sana sana watumishi wenzangu Kwa kunivumilia na kunielewa
katika kutimiza majukumu yangu. Zaidi nawashukuru sana wananchi naimani
nimejitahidi kuwatumikia Kwa moyo wangu wote na vipaji vyote na pale
niliposhindwa kutimiza ndoto yenu mnisamee"
Makonda aliendelea kufafanua na kutoa ahadi yake kwa wananchi kuwa
"Zaidi
nawaahidi nitaendelea kujituma zaidi ili niyaguse maisha ya kila mmoja
wetu kama ambavyo Serikali ya awamu ya 5 inavyokusudia. Mwisho si kwa
umuhimu ni Kwa wadau wa maendeleo naomba mfahamu kila cent mliyoitowa
ina thamani kwangu na kwa wananchi wangu. Tumefanya Mambo mengi na
hakika na tumegusa na hata kuleta faraja Katika maisha ya Watu wengi.
Kwakutambua mchango wenu ninaandaa siku ya kuwatambua na kuwatunuku tuzo
kama asante yangu kwenu"
Machi
13, 2016 Paul Makonda aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment