Msanii
wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap Harmorapa ameibuka na
kuiponda Albamu ya Diamond na kudai ni mbaya kama ilivyo sura yake.
Harmorapa
alijipatia umaarufu kwa kupenda kiki katika maswali kadhaa kuliko
muziki wake na leo ameibuka na jipya kuhusu Albamu mpya msanii wa Bongo
fleva Diamond Platnumz.
Albamu ya Diamond inayoitwa ‘A boy from Tandale’ imetoka rasmi jana usiku ambapo ilifanyiwa uzinduzi rasmi nchini Kenya.
Harmorapa kupitia ukurasa wake wa Instagram ameinanga Albamu ya Diamond na kudai ameitangaza sana alafu ametoa kitu kibovu:
"Bro
Chibu naye kelele nyingi za Albamu miezi saba mwisho wa siku anatutolea
albamu mbovu kama sura yangu sokwe, cha kukushauri Simba kama mkataba
wako wa karanga umeisha kaa dukani kwa dada yako Esma umsaidie kuuza
vitenge”.
Lakini
Harmorapa amejitamba na kudai kuwa albamu yake ambayo atakuja kuitoa
itakayoitwa Uthigawepathi itakuwa kali kuliko hiyo lakini pia amesema
albamu ya Ali Kiba itafunika kupita maelezo.
No comments:
Post a Comment