Akizungumzia
tukio hilo mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mwanza, Leonard Nundi amesema
tukio hilo limetokea jana Machi 13, saa kumi jioni ambapo wafuasi hao
wakiwa zaidi ya 500 walienda kuhani msiba huo na ghafla polisi
waliwavamia na kumtaka mfiwa kuongea naye.
“Chanzo
cha vurugu ni baada ya askari hao kuvamia msibani na kumhitaji mfiwa
ambaye ni Laurent Chiro kwa ajili ya mazungumzo, waliposhindwa kuelewana
walimchukua diwani na viongozi wengine waliokuwa meza kuu na
kuwapandisha kwenye gari la polisi,” amesema Nundi.
Amesema
wanachama waliokuwa msibani waliogomea kitendo hicho na kuanza
kuwarushia mawe polisi ambao nao walianza kujihami kwa kupiga mabomu ili
kuwatawanya.
Akizungumzia
tukio hilo, kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi pamoja na
kudai yuko wilayani Kwimba, lakini amesema wafuasi hao wamekuwa na
kawaida kukusanyika na kufanya vikao vyao vya kisiri.
Mmoja
wa wanachama aliyekuwa eneo la tukio, Emmanuel Tumbo amesema wafuasi
hao wametoka katika kata zote 18 za Jiji la Mwanza ambao wamejiwekea
utaratibu wa kuhani misiba inapotokea kwa mwanachama anayefiwa au
kufariki dunia.
No comments:
Post a Comment