Akizungumza Juzi 11 Machi 2018 na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara katika Kitongoji cha Mahiga, Kijiji na Kata ya Mwakitoliyo, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Naibu Waziri wa wizara ya madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb) amekiri kuwa zipo changamoto katika jambo hilo hivyo serikali itapitia upya tathimini sambamba na ulipaji wa fidia ili kuhuisha sintofahamu hiyo iliyopelekea wananchi hao kupaza sauti zao za malalamiko.
Mhe Biteko alisema kuwa katika sekta ya madini mnufaika wa kwanza lazima awe mtanzania kwani sheria ya madini ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2017 inaelekeza kuwa na uchumi fungamanishi kwa wananchi ili kuinua pato la wananchi sambamba na mchango wa sekta ya madini kwenye Pato la Taifa.
Wakazi
wa Kitongoji cha Mahiga, Kijiji na Kata ya Mwakitoliyo, Halmashauri ya
Wilaya ya Shinyanga wakimsikiliza Naibu waziri wa madini Mhe Doto
Mashaka Biteko (Mb) wakati wa mkutano wa hadhara, Juzi 11 Machi 2018.
Aidha, Mhe
Biteko aliwasihi wananchi hao kuwa watulivu katika kipindi kifupi
ambacho serikali inapitia upya tathmini hiyo huku akiwasihi kuacha
uvamizi katika eneo hilo kwani kufanya hivyo ni uvunjifu wa sheria,
kanuni na taratibu za nchi.“Ndugu zangu wananchi sio kweli kwamba wawekezaji ni wabaya lakini wanapaswa kutambua tu wakija kuwekeza nchini wanapaswa kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi ikiwa ni pamoja na kuwa na mahusiano mazuri na wananchi wanaoishi karibu na mradi huo,” alikaririwa Biteko (Mb)
Machi 10, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wananchi katika eneo la Nyasubi katika Halmashauri ya mji wa Kahama Mkoa wa Shinyanga wakati wa dhifa ya uzinduzi wa barabara ya Isaka-Ushirombo yenye urefu wa Kilomita 132, alimuagiza Naibu Waziri wa wizara ya madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb) kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe Ahmed Salum kufanya ziara na kuwasikiliza wananchi kuhusu malalamiko hayo ili serikali kutafuta ufumbuzi wa haraka.
Wananchi hao wanalalamikia kufanyiwa tathmini tofauti na matakwa ya sheria huku wakipatiwa malipo kiduchu pasina kufanyika mkutano wa hadhara wa maridhiano baina ya wananchi na muwekezaji huhu wakiomba kufanyika upya tathmini ya maeneo yao.
Na Mathias Canal, Shinyanga
No comments:
Post a Comment