Mafunzo hayo siku mbili yanaliyofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma yamejumuisha wajumbe wa Menejimenti, Kamati ya Ukaguzi na Wakaguzi wa Ndani ya Wizara hiyo. Wawezeshaji wa Mafunzo hayo ni Bwa. Alphonce Muro na Bw. Athanas Pius kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, katika Ofisi ya Idara ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani.
Washiriki wa mafunzo hayo wamesisitizwa kuzingatia utatu (Menejimenti, Kamati ya Ukaguzi na Wakaguzi wa ndani) katika utekelezaji wa majukumu yao ya kuhakiki, kusimamia na kudhibiti utendaji mahali pa kazi ili kuongeza thamani ya huduma na kazi za kila upande katika kufanikisha malengo ya Wizara. Akitoa mada kwa washiriki wa mafunzo hayo mwezeshaji alisema,
“Uhusiano na mawasiliano kati ya watendaji hao ni muhimu katika kufanikisha maelengo ya Wizara”.. amesema Bw. A. Muro
Imeelezwa kuwa kila upande una wajibu wa msingi katika kuchangia kufikiwa kwa malengo ya Wizara, washiriki wamesisitizwa kuwa na mawasilino na kushirikiana katika kupokea na kutekeleza ushauri wa kitaalam unaotolewa na maafisa wa kitengo cha Ugaguzi na Kamati ya Ukaguzi wa Ndani kwa lengo la kuboresha utendaji na usimamizi.
Akiwasilisha mada ya Majukumu ya kamati ya Ukaguzi ya Wizara, mtoa mada Bw. Athanas Pius amebainisha kuwa maafisa wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Wizara wanawajibu wa kutoa ufafanuzi wa masuala ya kitaalam ambayo yalishirikisha wataalam wa fani mbalimbali katika uhakiki na uandishi wa taarifa husika. Maelezo hayo ya ushauri wa kitaalam yanatajwa kuwa ni ushauri au mapendekezo lakini kimsingi ni maagizo ya wataam wa eneo husika na yanahitaji utekekezaji wake ili kuongeza thamani katika utendaji, usimamizi na uadilifu mahala pa kazi.
Kadhalika, mtoa mada amesisitiza kufanyika kwa tathmini ya mwaka ya utendaji kazi ya kamati ya ukaguzi ya Wizara na pia kila mjumbe mmoja mmoja ili kubaini mchango na ushiriki wa wajumbe katika kumsaidia Wizara kufikia malengo yake ya kuwa maendeleo jumuishi kwa kila mwananchi. Mafunzo hayo yatahitimishwa leo jioni tarehe 13 Machi 2018.
No comments:
Post a Comment