Serikali
kupitia, Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji wa Thamani na
Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF), imetekeleza maombi 5 ambayo
yanawasaidia wafugaji hao kuongeza thamani ya mifugo yao kupitia Soko
la Kimkakati la mifugo Longido lililojengwa na Program hiyo.
Mwishoni
mwa mwaka 2017, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,
Ajira ,Kazi, Vijana na Watu wenye Ulemavu ) Mhe.Jenista Mhagama,
alikuwa na ziara ya kukagua ujenzi wa soko hilo wilayani humo, ambapo
baada ya ukaguzi alikutana na wafanyabiashara ya mifugo, ambao
waliwasilisha maombi 5, ambayo yangeweza kuongeza Thamani Biashara za
Mifugo na kutatua kero zote za wafanyabiashara wa mifugo wilayani
humo.
“Serikali
ya awamu ya tano imeamua kuwasikiliza watu wanyonge na ambao wanajituma
kuchapa kazi, lakini pia lengo la Program ya MIVARF ni kuongeza kipato
kwa wananchi hasa waishio vijijini, kwa mantiki hiyo nilimuelekeza
Mratibu wa Program Kutekeleza maombi yao haraka sana ili wafugaji hawa
wapate tija ya ufugaji kupitia soko hili” alisema Mhagama
Mwenyekiti
wa wafanyabiashara wa Mifugo wilayani Longido, Saruni Laizer amesema
maombi waliyowasilisha serikalini ili waweze kupata tija ya mifugo
kupitia soko la Kimkakati la Mifugo Longido yamefanyiwa kazi na Program
ya MIVARF ndani ya miezi mitatu tangu wayasilishe, ikiwa ni; Mizani ya
kupima mifugo, Maji ya kunyweshea mifugo, machinjio, Josho, pamoja na
umeme.
“Tulihitaji
maji hapa ili mifugo isije ikafa wakati inasubiri kuuzwa kwa kukosa
maji, lakini umeme hapa ni muhimu kwani biashara zetu zinafanyika usiku,
tayari hadi jenereta imeletwa kwa ajili ya kuhakikisha biashara
haikwami kwa dharura yoyote ile, lakini mizani itasaidia kutowauza
mifugo kwa kuangalia kwa macho bali kwa uzito wao” alisema Laizer
Mhagama
alitoa maagizo hayo baada ya kukagua Soko la kimkakati lililojengwa na
Serikali kupitia Ofisi Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Programu ya Miundo
mbinu ya Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini
(MIVARF).
Soko
hilo litawanufaisha wananchi wapatao 14,2000 wa wilayani Longido
ambapo asilimia 95 ni wafugaji na wanaojishughulisha na biashara za
mifugo.
Soko
hilo la kimkakati ambalo halijafunguliwa rasmi , tayari halmashauri ya
wilaya hiyo imeweza kukusanya mapato ya kiasi cha shilingi milioni 106
kwa mwaka 2016/2017 ambapo kwa makusanyo hayo yamewezesha halmashauri
hiyo kuvunja rekodi ya miaka kumi iliyopita kwa kukusanya shilingi
bilioni 1.3 kwa mara ya kwanza kwani awali mapato yake yalikuwa chini
ya bilioni moja.
MIVARF;
ni Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko na Huduma za Kifedha Vijijini
iliyobuniwa na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Mfuko wa
Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo yaani (IFAD) na Benki ya Maendeleo ya
Afrika (ADB). Programu hii inatekelezwa katika mikoa 29 ya Tanzania
Bara na Tanzania Visiwani tangu mwaka 2011.
Sehemu
ya kunyweshea mifugo iliyojengwa katika Soko la Kimkakati la
Longido, Wilayani Longido kwa ufadhili wa Programu ya Miundo mbinu ya
Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).
Baadhi
ya mifugo wakiwa katika eneo la kunywa maji kablaya kuuzwa katika Soko
la Kimkakati la Longido, Wilayani Longido ambalo limejengwa kwa
ufadhili wa Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji wa Thamani na
Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).
No comments:
Post a Comment