Kampuni
ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) imeandaa shindano
la kuimba wimbo wa MO Margarine kwa wanafunzi wa elimu ya msingi na
sekondali, linalokwenda kwa jina la ‘MO Margarine Star’.
Akizungumza
kuhusu shindano hilo, Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji
ametoa masharti ya shindano hilo, kwamba kabla ya mwanafunzi kushiriki
shindano hilo anatakiwa apate ridhaa kutoka kwa wazazi ama walezi wake.
Ameeleza
kuwa, ili kushiriki shindano hilo, mwanafunzi anatakiwa ajirekodi video
akiimba wimbo huo, na kuposti katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii
wa Instagram au Facebook kisha kuishirikisha akaunti ya METL
inayopatikana na kuweka hashtag ya #MoMargarineStar.
Dewji
alisema zawadi kwa washindi ni Sh. 700,000 kwa mshindi wa kwanza, Sh.
600,000 kwa mshindi wa pili, Sh. 500,000 kwa mshindi wa tatu na kuanzia
mshindi wa nne hadi 10 watapewa Sh. 400,000 kwa kila mmoja.
No comments:
Post a Comment