Viongozi
wa Chadema waliotakiwa kuripoti kituo kikuu cha polisi leo Jumanne
Machi 13, 2018 wametakiwa kufika tena kituoni hapo Machi 16, 2018.
Licha
ya kutakiwa kuripoti viongozi saba, waliofanikiwa kufika kituoni hapo
ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji na naibu Katibu Mkuu wa
chama hicho Zanzibar, Salum Mwalimu.
Viongozi
wengine watano akiwemo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe
wameshindwa kuripoti kutokana na kuhudhuria vikao vya Kamati za Kudumu
za Bunge vilivyoanza leo mjini Dodoma.
Kufuatia hali hiyo, wametakiwa kuripoti Machi 16, saa 2:00 asubuhi.
Akizungumza
na waandishi wa habari nje ya kituo hicho Dk Mashinji amesema,
“Viongozi wote wameshatoa maelezo yao. Leo tumeripoti wawili na viongozi
wengine ni wabunge na wapo Dodoma walishindwa kujigawa katika mambo
mawili.”
No comments:
Post a Comment