Viongozi
watatu wa nafasi za juu katika Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP)
wameitikia wito wa kufika kwa mpelelezi wa makosa ya Jinai (DCI) Jijini
Dar es Salaam leo asubuhi kwa lengo la kuhojiwa kutokana na tukio la
Abdu Nondo.
Hayo
yamebainishwa na taarifa iliyotolewa na Afisa Habari- TSNP, Hellen
Sisya baada ya kupita siku moja tokea Jeshi la Polisi kupitia Kamanda wa
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa kuwataka
viongozi hao kufika katika ofisi za DCI.
"Tumepokea
taarifa ya Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam inatofautiana
kabisa na ile ya Iringa juu ya kuonekana kwake. Hata hivyo, kabla ya
taarifa ya uchunguzi kulitanguliwa na matamko ya viongozi wa juu
waliodai kuwa Abdul Nondo alijiteka mwenyewe jambo ambalo kwa vyevyote
lingeathiri uchunguzi wa jeshi la polisi", amesema Hellen.
Pamoja
na hayo, Hellen ameendelea kwa kusema "pamoja na mapungufu yote
tunaamini Nondo atatendewa haki atakapofikishwa mahakamani".
No comments:
Post a Comment