Jeshi
la Polisi Mkoa wa Kigoma limesema watu wawili wanaotuhumiwa ni
majambazi wameuawa wakati wakijibizana kwa risasi na Polisi.
Pia
limesema limekamata silaha mbili AK 47 zenye namba UB38341997 na risasi
17 ndani ya magazine na AK47 1967TY4577 na risasi 24 ndani ya magazine
pamoja na pembe za ndovu vipande 9 katika pori la Makerema wilayani
Kasulu.
Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Maltin Otieno leo
wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari na kusema ilipofika
majira ya saa 5:00 usiku wa Machi 19, 2018 kwenye pori la Makere
katika Kijiji cha makere wilayani Kasulu watu wawili ambao ni Norbert
Andrew na Bukuru Stiven ambaye ni mkimbizi kambi ya Nyarugu waliuawa kwa
kushambuliwa na majambazi wenzao wakati wakienda kuwaonesha Polisi
silaha ambazo walikuwa wamezificha porini.
Amesema
watu hao walikamatwa katika tukio moja la kuvunja kibanda na kuiba na
mmoja wa majambazi hao waliangusha simu eneo la tukio iliyowezesha
polisi kumkamata.
"Baada
ya kuhojiwa na polisi waliwataja wenzao na kufanikiwa kuwakamata
wanne.Katika mahojiano walikiri kuhusika na matukio ya mauaji na
uvamizi katika nyumba za watu wilayani hapo.
"Hata
hivyo baada ya mahojiano hayo mtuhumiwa aliwaongoza Polisi mpaka kambi
ya Nyarugusu na kufanikisha kukamatwa mtuhumiwa mwingine na baada ya
kupekuliwa alikutwa na silaha walizokuwa wakizitumia kufanya
uhalifu,"amesema.
Amesema baada ya kukutwa na silaha hizo alieleza kuna silaha nyingine tano amezificha porini,hivyo polisi waliondoka na watuhumiwa hao na walipofika maeneo ambayo wameficha silaha ndipo risasi zilianza kupigwa na majambazi wenzao.
Amesema baada ya kukutwa na silaha hizo alieleza kuna silaha nyingine tano amezificha porini,hivyo polisi waliondoka na watuhumiwa hao na walipofika maeneo ambayo wameficha silaha ndipo risasi zilianza kupigwa na majambazi wenzao.
Aidha
Kamanda Otieno amewaomba wakimbizi wote wenye silaha katika kambi za
wakimbizi kuzisalimisha polisi kabla ya Machi mwishoni na baada ya hapo
watanzaa msako kupitia kamati ya ulinzi na usalama na mkoa huo.
No comments:
Post a Comment