TAARIFA YA MKUU WA MKOA DAR ES SALAAM KUHUSU TUKIO LA KUSHAMBULIWA KWA AFISA UBALOZI WA SYRIA.
Kama
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar Es Salaam
nimeshtushwa na taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba
Afisa Ubalozi wa Syria ameshambuliwa na kuporwa kiasi kikubwa cha fedha
leo mchana Jijini Dar Es Salaam. Taarifa hiyo imeenda mbali zaidi na
kusema kwamba Dar Es Salaam sio salama na kueleza watu wawe makini
zaidi.
Nawaomba
sana wananchi wa Dar es Salaam muendelee kuwa watulivu na mkielewa
kwamba Mkoa wenu ni salama salama sana. Vyombo vya usalama vinalifanyia
kazi tukio hili na taarifa za awali nilizopokea zinaonyesha tukio hili
linaweza kuwa limepangwa na watu wa ndani. Tunafuatilia zaidi kujua kwa
nini Afisa huyo hakuomba ulinzi wa polisi akiwa amebeba kiasi hicho
kikubwa cha fedha na pia kwa nini dereva wake amekimbia.
Kwa
hali ilivyo mpaka sasa kuna uwezekano ikawa ni tukio la kupangwa na
watu wa ndani. Hatutaruhusu watu wachache wachafue taswira ya Mkoa wetu.
Uchunguzi
ukifikia sehemu nzuri taarifa rasmi itatolewa na vyombo vyetu vya
usalama. Ulinzi na usalama wa wananchi wetu ni muhimu sana.
Mh. Paul Makonda
Mkuu wa Mkoa Dar Es Salaam
No comments:
Post a Comment