Baada
ya kuvuja kwa video inayowaonyesha wanamuziki wa Bongo Fleva, Faustina
Charles ‘Nandy’ na Billnas wakiwa faragha na ambayo imezua gumzo jan
katika mitandao ya kijamii, Nandy amekiri kwamba video hiyo ni ya kweli
japo ni ya mwaka 2016 na amewaomba msamaha Watanzania kwa walioiona
video hiyo. Leo amefika Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kujieleza na
baada yakutoka kasema haya kupitia akaunti yake ya instagram;-
”Kiukweli
niko katika wakati mgumu wa maisha yangu.. jana sikuwa sawa ila leo
nimeweza hata shika simu yangu najuaa matusi yote na fedhea kutoka kwa
mashabiki wangu ni sababu wanaamini hili ni kusudio letu au langu hii
video iwe public naapa na naumia sana sana kwa hili lilitokea!!!
sihusiki na kusambaza video wala siwezi ruhusu kitu kama hichi kitokee
kwenye maisha yangu ya usanii hata ya kawaida!
Sitakiwi
kujieleza sana ila naamini nikiandika hili nitakaa na amani kwa ambaye
ataamuaa kuendelea kuni hukumu aendelee tu kunihukumu kwani kweli
nimekosea ila ajiulize kama yeye hajawahi kukosea! Mambo yetu wote ya
private yanatakiwa kubaki private, aliyeyatoa amefanikiwa kuleta hii
taharuki, sintofahamu na maumivu makubwa ambayo sijawahi kupata maishani
mwangu. ilaa Naamini sababu kuu ya hii video kuwa out ni mambo ya simu
zetu ambayo inaweza kumtokea mtu yoyote!! nilibadili simu yangu mara 2
toka 2016 na bilnas aliibiiwa simu yake huko nyuma, kwa mujibu wake, so
hatujui mpaka sasa imetoka kwa simu ya nani? maswali ni mengi matusi ni
mengi simu na sms ni nyingi mnoo… naumiaa naumiaa kupita kiasi.
Kanisaa
langu, wazazi wangu, ndugu zangu, marafiki zangu wa karibu wameliaa
sana sanaa mnoo!!! sikatai nimerecord video na nilikuwa kwenye mahusiano
na nilifanya kwa mapenz ila siwez weka public, Mungu anisamehe kwa
niliyowakwaza. nimepoteza watu wa maana nahisi ku poteza vitu vingi ilaa
nashukuru sana kwa watu wangu wa karibu waliolia na mimi mashabiki
wanaoniamini Mimi na dhamira yangu ya kweli, marafiki walio liaa kwa
ajili yangu nawashukuru sana mnoo yote naomba radhi sana sanakwa kilicho
tokea haikuwa kusudio langu na naumiaa sana!!! asante sana basata kwa
ushirikiano wenu kwakuwa na mm na kunipa moyo hii ni fundisho kwa wote
nimejifunza kitu kikubwa sana!! mashabiki, kabisa langu, serikali yangu
viongozi wenye imani na mimi, mashabiki zangu, ndugu jamaa na marafiki.
naomba Nisameheni naamini na hili nalo litapita. Sitaongea tena kwenye
vyombo vya habari kuhusu hili namwachia Mungu, pale roho yangu
itakapopata wepesi tutaonana tena kwenye Sanaa. Naomba mniombee nipate
wepesi wa kuvuka hili daraja.๐๐ผ”
No comments:
Post a Comment