Mwenyekiti
wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Katibu wake, Dk. Vincent Mashinji
wameondoka katika Kituo Kikuu cha Polisi central baada ya kuripoti, huku
Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya ikidaiwa atalala mahabusu kwa
ajili ya kufikishwa mahakamani.
Wengine waliondoka kituoni hapo ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu.
Akizungumza
na waandishi wa Habari, Mashinji amesema kuwa wameripoti kituoni hapo
kama walivyoamriwa na mahakama, lakini wameambiwa Mbunge Bulaya atabaki
mahabusu kwa ajili ya upelelezi.
“Mbunge Bulaya amebaki mahabusu kwa sababu za kiupelelezi lakini tumeambiwa ataunganishwa katika shauri letu,” -Dk.Mashinji.
No comments:
Post a Comment