Muigizaji
wa Bongo movie na mfanyabiashara Jacqueline Wolper amefunguka na kusema
kuwa hataweza kukaa na kusapoti kazi za Harmonize sababu anamuonea
huruma mpenzi wake Sarah.
Siku
chache zilizopita Wolper alitengeneza headlines kwenye mitandao ya
kijamii baada ya yeye na mpenzi wa Harmonize Sarah kurushiana vita ya
maneno kwenye Instagram.
Ambapo
Sarah alimtaka Wolper aache kumtumia Meseji za kumtaka Mpenzi wake
Harmonize jambo ambalo lilimkera Wolper kwani aliweka wazi kuwa akaunti
yake ya Instagram ilidukuliwa hivyo hakuwa yeye aliyekuwa anatuma
Meseji.
Kwenye mahojiano aliyofanya leo na Sam Misago Wolper amesema kuwa ameamua kuacha kabisa kusapoti kazi za Harmonize:
'Mimi
sio mswahili na wala sina uswahili tulianza mapenzi kwa mimi kusapoti
kazi zako,` lakini sasa naona ili nisikwaze mahusiano yako naona bora
nisisapoti kazi za Harmonize kwa sababu yule mwanamke wake anahitaji
kuhurumiwa”.
Lakini pia Wolper amesisitiza kuwa amefikia uamuzi wa kumblock Harmonize na Sarah kwenye Instagram ili aepushe maneno maneno.
No comments:
Post a Comment