Diwani
wa Viti Maalumu (CCM) wilaya ya Morogoro, Zuhura Mfaume amefariki dunia
jana baada ya kuugua maradhi ya tumbo kwa muda mfupi na anazikwa leo,
Tarafa ya Matombo wilayani humo.
Akitoa
taarifa za kifo cha diwani huyo mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Sudi
Mpili amesema Zuhura alifariki jana (Aprili 12) mtaa wa Karume Manispaa
ya Morogoro ambako alikuwa akiugua kwa ndugu zake.
Mpili
amesema kuwa marehemu Zuhura enzi za uhai wake alikuwa akiwasaidia sana
akinamama na wananchi wa wilaya ya Morogoro kwa kuwawakilisha vyema
katika vikao mbalimbali vya maamuzi.
Naye
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Kibena Kingo amesema kuwa marehemu
Zuhura amedumu kwenye baraza la madiwani katika awamu mbili na alikuwa
mtulivu na msikivu katika vikao mbalimbali.
Kingo
amesema kuwa marehemu Zuhura alikuwa mtu mwenye msimamo na
asiyeyumbishwa hivyo kila alichokuwa akichangia kilikuwa na mchango na
mslahi kwa wananchi.
Kwa
upande wake Diwani wa Viti Maalumu CCM, Jesca Mbondo amesema kuwa pengo
aliloacha marehemu Zuhura haliwezi kuzibika kwani mbali ya kuwa diwani
lakini pia alichukua nafasi kama mama na mlezi kwenye jamii na vikundi
mbalimbali.
No comments:
Post a Comment