Shirika
la Ndege nchini ATCL limeondolewa katika mfumo wa malipo wa Shirika la
Kimataifa la Usafiri wa Anga IATA kutokana na kukabiliwa na madeni na
sasa limetiliana saini ya makubaliano ya miaka mitano na Kampuni ya
Ndege ya HAHN Air kuuza tiketi za Air Tanzania.
Akizungumza
na wanahabari huko Zanzibar, Mkurugenzi wa ATCL Mhandisi Ladislaus
Ernest Matindi, amesema wamelazimika kuingia kwenye makubalianao na
kampuni hiyo ili wasikose baadhi ya huduma za malipo ya tiketi.
"Tuna
madeni, sikumbuki yalifikia kiasi gani lakini ni madeni makubwa ambayo
yalilazimisha kusimamishwa uanachama au kufungiwa huduma hizi mpaka
tutakapokuwa tumelipa hayo madeni.
"Kubwa
zaidi ilikuwa ni sisi kuwa katika mfumo wa shirikisho wa mashirika ya
ndege dunia IATA ambayo ndo mfumo wa uuzaji na utawanyaji wa Tiketi.
Maana mabadilishano ya pesa au kupeleka pesa kutoka shirika moja kwenda
lingine hufanyika kwa kutumia huo mfumo wa IATA. Hii tunaanza kufanya ni
kupitia kwakweli mgongoni kwa mtu.
No comments:
Post a Comment